Ticker

6/recent/ticker-posts

CHELSEA NAYO YAJITOSA KATIKA HARAKATI ZA KUMNYAKUA WILLIAN

Chelsea iko katika mazungumzo ya kujaribu bahati yao ya kupata saini ya mchezaji aliye katika malengo ya timu ya Tottenham  WILLIAN kutoka Anzhi Makachkala.
Chelsea nayo imetumbukia katika vita vya kutaka saini ya Wilian Anzhi Makachkala.
 klabu hiyo ya darajani imejiingiza katika vita hiyo baada ya
wapinzani wa kutoka London Tottenham kuwa na  mazungumzo na WILLIAN mapema jana Alhamisi.
Spurs walikuwa tayari wameshaweka mzigo wa  £ 30m juu ya kiungo huyo,ambaye pia  ali ahidiwa  mkataba wa miaka mitano kama atatua White Hart Lane. 
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye pia alikuwa anahusishwa na kijiunga Liverpool mapema katika majira  haya ya joto, inaonekana bado hajatoa msimamo wake na kua muwazi. 
Akiwa uwanjani utamtaka!
Chelsea tayari wameshasajili katika dirisha hili la usajili,akiwemo mchezaji Andre Schurrle  kutoka Bayer Leverkusen kwa £ 18m,pamoja na Marco van Ginkel kwa  £ 8m kutoka Vitesse Arnhem

Post a Comment

0 Comments