Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kumaliza tofauti na baadhi ya wajumbe wa baraza la wadhamini ambao walikua wanapinga
mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa kiuongozi.
Khamisi kilomoni pamoja na wajumbe wenzake wa baraza la wadhani walipinga hadharani mchakati huo ambao tayari umeshafanyiwa marekebisho kikatiba ya kuitoa Simba kujiendesha kwa mfumo wa uwanachama na kuingia katika mfumo wa hisa.
Rais wa klabu ya Simba Evance Aveva amethibitisha kumaliza kwa tofauti hizo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi jijini Dar es salaam.
Aveva amesema wamekaa chini ya baadhi ya wajumbe hao wakiongozwa na Khamis Kilomoni na wamekubaliana kumnaliza tofauti zilizokuwepo kwa maslahi ya klabu ya Simba.
Kwa upande wa muwakilishi wa baadhi ya wajumbe wa baraza la wadhamini wa klabu ya Simba Khamis Kilomoni amesema hatua ya kuafikiana na uongozi wa juu, yamewapa faraja na wametoa baraka ya msuala mengine kuendelea.
Hata hivyo Kilomoni akatoa angalizo kwa baadhi ya wanachama wa klabu ya Simba ambao walijiingiza kwenye mzozo wa kutangaza hadharani kutolitambua baraza la wadhamini kufutia mvutano uliokua ukiendelea.
Khamisi kilomoni akafichua ya moyoni kuhusu msimamo wake na wajumbe wengine ambao walikua wakipinga mchakato wa mabadiliko, kwa kusema wataendelea kuilinda Simba na mali zake.
0 Comments