Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.DEC 13.2016 SAA 02:11 USIKU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amewapongeza viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC),
waliochaguliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu
uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika salamu zake za kuwapongeza viongozi hao, Rais Malinzi amesema
huu ni wakati mwafaka wa kujipanga katika kufuzu michuano ya kimataifa
tukianzia hii Olimpiki ya mwaka 2020 itakayofanyika Tokyo, Japan.
Kuonyesha namna TFF ilivyopjipanga kwa ajili ya maandalizi hayo,
msimu huu imeendesha Ligi Kuu ya Soka Taifa kwa upande wa wanawake na
wavulana wenye umri wa chini ya miaka 23, lengo likiwa ni kupata timu ya
kutafuta kufuzu.
Tumewaomba wanafamilia wa mpira wa miguu kupendekeza majina majina ya
timu za taifa za wanawake na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 23
kabla ya timu hizo hazijaingia kwenye kalenda ya kutafuta timu za kufuzu
kwa kushirikiana na TOC.
Kwa Malengo yote hayo na mengine, TFF inaahidi kushirikiana na TOC na
vyama vingine vya michezo kikiwamo cha riadha ambacho pia kimepata
viongozi wake hivi karibuni.
TFF inaamini itapata ushirikiano wa kutosha kutoka timu nzima ya
Viongozi wa TOC watakaoongoza kwa miaka minne ijayo, kuanzia sasa hadi
kipindi cha Olimpiki ya Tokyo 2020 ambao ni Rais Gulam Rashid aliyepata
kura za ndiyo 48 na mbili za hapana na Makamu wa Rais, Henry Tandau
aliyepata kura za ndiyo 44, tano zikimkataa na moja ikiharibika.
Wengine ni Katibu Mkuu, Filbert Bayi aliyetetea kwa kishindo nafasi
yake hiyo baada ya kupata kura za ndiyo 49, huku hapana moja huku Katibu
Msaidizi Suleiman Mohamed Jabir akichomoza kwa kura 49 huku moja
ikimkataa na Mweka Hazina ni Charles Nyange kura za ndiyo 47 huku hapana
ni tatu na Mweka Hazina Msaidizi alichaguliwa Juma Khamis Zaidy kura
47, moja ikiharibika na hapana ni mbili.
Katika uchaguzi huo ulioendeshwa na kufanyika kwa utulivu mkubwa,
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Uchaguzi, Wakili Lloyd Nchunga, aliwataja
walioshinda nafasi tano za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji kutoka Bara na
kura zao kwenye mabano kuwa ni Irene Mwasanga (50), Noorelain Sharrif
(48), Muharam Mchume (39), Amina Lyamaiga (32), na Donath Massawe (30).
Kwa upande wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Zanzibar walishinda ni
Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, Nasra Juma Mohamed
(44), Katibu wa Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA), Suleiman Ame Khamis
(42), Mussa Abdulrabi Fadhi (37), Ramadhan Zimbwe Omar (33), na Sheha
Mohammed Ali (30).
Kwa upande wa Wana Olimpiki, Mwanariadha wa kike, Zakia Mrisho
alishinda kwa kura 49, Samuel Mwera kura 48 na Fabian Joseph kura 44.
Nafasi za juu ambazo zilikuwa na mgombea mmoja mmoja.
0 Comments