Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.OCT.21,2016 SAA 12:44 JIONI
Wakati mzunguko wa tano wa Ligi Daraja la Kwanza ukitarajiwa
kuendelea kesho Jumamosi na keshokutwa Jumapili, Bodi ya Ligi
ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeagiza makamishna na
wakuu wa vituo kuzuia wachezaji wote ambao hawana leseni kutocheza.
Hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14 (16), inayosema: “Wachezaji wote
watatambulika kwa kutumia leseni zao zitakazotolewa na kuidhinishwa na
TFF. Mchezaji yoyote ambaye hatakuwa na leseni hataruhusiwa kucheza
katika mchezo husika.”
Kipindi cha dharura amvacho TFF ilikitoa ni kwa mizunguko mitatu ya
mwanzo, lakini taarifa za makamishna zinaonyeha kuwa raundi ya nne bado
kuna timu zilikuwa zinatumikia leseni za muda ilihali walikwisha
kutaarifiwa kuwa leseni zao ziko tayari na wao wanakwama kuzifuata hapa
TFF. Kuanzia sasa hakuna sababu yoyote itakayotolewa na ikaeleweka kwa
mchezaji ambaye hatakuwa na leseni.
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza, michezo ya Kundi A
kesho itakuwa ni kati ya Pamba ya Mwanza na African Sports ya Tanga
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Dar es Salaam kutakuwa
na ‘Mbezi Derby’ ambako Kiluvya United itacheza na Mshikamano kwenye
Uwanja wa Karume, Ilala.
Katika kundi hilo, Friends Rangers pia ya Dar es Salaam, itacheza na
Lipuli ya Iringa Jumatatu kwenye uwanja huo wa Karume, Dar es Salaam
wakati Jumanne Oktoba 25, 2016 Polisi Dar itacheza na Ashanti United ya
Ilala. Mchezo huo pia utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Mbeya Warriors ya Mbeya na Coastal
Union ya Tanga; Kemondo itacheza na Mlale ilihali Polisi Moro itacheza
na Kurugenzi ya Iringa wakati Jumapili Oktoba 23 KMC ya Kinondoni, Dar
es Salaam itacheza na Mji Njombe.
Kwa upande wa Kundi C michezo yote minne itachezwa
kesho Oktoba 22, mwaka huu ambako Singida United itacheza na Polisi
Dodoma kwenye Uwanja wa Namfuta mjini Singida; Rhino itapambana na
Alliance ya Mwanza kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora huku
Mgambo JKT itakuwa mwenyeji wa Mvuvumwa ya Kigoma kwenye Uwanja wa
Mkwakwani mjini Tanga.

0 Comments