Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.19,2016 SAA 12:00 JIONI
Baada ya kuifunga Congo-Brazzaville mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza
kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika,
timu ya taifa
Serengeti inatarajiwa kuondoka Alhamisi wiki hii kwenda kupiga kambi nje
ya mipaka ya Tanzania.
Hata hivyo, taratibu zinapangwa kuhakikisha kwamba timu hiyo
inakwenda kupiga kambi kwenye nchi tulivu inayolingana hali ya hewa na
Congo Brazzaville kadhalika chakula pamoja na mazingira. Tanzania na
Congo Brazzavile, zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo
Brazzaville na timu itakayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili
itafuzu kwa fainali hizo.
Katika mchezo uliofanyika jana Septemba 18, 2016
timu hiyo ya Tanzania maarufu kwa jina la Serengeti Boys ilipata mabao
yake kupitia Yohana Mkomola na Abdi Makamba wakati yale ya Congo
yalifungwa na Langa-Lesse Percy na Makouana Beni ambao mashabiki wa soka walikuwa wakiwalalamikia kuwa ni “wakubwa.”
Ili ifuzu kwa fainali zitakazofanyika mwakani huko Antananarivo,
Madagascar katika fainali zitakazoanzia Aprili, 2017, Serengeti Boys
inatakiwa ibaki na matokeo yake ya sasa na ihakikishe inapata ushindi na
kama sare basi wapate bao kufuta faida ya bao la ugenini ambalo Congo
Brazzaville walikuwa wanasheherekea baada ya mchezo.

0 Comments