Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.19,2016 SAA 12:11 JIONI
Ivory Coast imeiondoa
Tanzania katika mchezo wa mpira wa miguu wa ufukweni baada ya kushinda
kwa mabao 6-4, lakini wamebaki
na jina la Kipa Na. 1 wa timu ya
Tanzania, Juma Kaseja wakisema: “Angekuwa tangu mwanzo, wangekuwa na
wakati mgumu.”
Kaseja alikuwa kikwazo kwa Ivory Coast katika mchezo uliofanyika
Jumamosi iliyopita huko jijini Abdijan ambako wenyeji walitamba kwamba
wangeshinda mabao mengi, lakini kikwazo kilikuwa Kaseja na wakahoji
wenyeji wa Tanzania: “Anacheza timu gani Tanzania, au mmemtoa nje ya
nchi?”
“Kaseja alicheza kwa umahiri na kuzuia michomo mingi kutoka kwa
washambuliaji wa Ivory Coast, na mabao aliyofungwa yalikuwa ni kwa
bahati mbaya,” amesema Kocha Mkuu wa timu hiyo, John Mwansasu mara baada
ya kurejea kutua jijini Dar es Salaam leo alfajiri.
Tanzania imeondolewa kwa jumla ya mabao 13-7 baada ya mchezo wa
kwanza uliofanyika hapa nyumbani kupoteza kwa mabao 7-3. Michezo hiyo ni
ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa soka la
ufukweni ambako fainali zake zitafanyika jijini Lagos, Nigeria Desemba,
mwaka huu.
TFF imepanga kuhakikisha kwamba inaboresha soka la ufukweni baada ya
kutengeneza uwanja maalumu wa mchezo huo ulioko kando ya Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.

0 Comments