Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:WABUNGE SIMBA NA YANGA KUKIPIGA TAIFA JUMAPILI,BONGO FREVA NA BONGO MOVIE PIA

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.20,2016 SAA 12:11 JIONI

Wabunge wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania wametangaza mpango wao wa kucheza mchezo maalum
ambao utasaidia kuchangi fedha kwa ajili ya janga la tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani Kagera juma lililopita.
Mwenyekiti wa timu ya Bunge William Ngeleja akizungumza
Mwenyekiti wa timu ya Bunge William Ngeleja amesema katika kuhakikisha lengo lao linatimia wameamua kucheza mchezo maaluma mbao utawahusisha wabunge wanaozishangilia klabu kongwe hapa nchini za Simba na Yanga ili kuleta chachu ya ushindani.

Amesema dhumuni lao linapaswa kuungwa mkono na watanzania kwa kwenda uwanjani kushuhudia mchezo huo maalum, ambao kwa upande mwingine utatoa burudani.
Single Mtambalike (Rich Rich) akizungumza

Kwa upande wa muwakilishi wa timu ya wasanii wa filamu (Bongo Movie) Single Mtambalike (Rich Rich) ametoa wito kwa watanzania bila kujali itikadi za kimichezo kufika uwanjani siku ya jumapili kwa lengo la kushuhudia burudani pamoja na kuchangia sehemu ya fedha zitakazowasaidia waathirika wa janga la tetemeko la ardhi.

Pia mewataka wasanii wenzake kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii ili kuwavuta watu wengine wa ndani nan je ya nchi ili waweze kufika uwanjani siku hiyo, kwa lengo la kuonyesha umoja na mshikamano kwa kuwasaidia watanzania waliofikwa na matatizo.
Karama Masoud (Kalapina) akitamba
Naye kocha mchezaji wa timu ya wasanii wa muziki (Bongo Fleva) Karama Masoud (Kalapina) ametamba kuwa na kikosi kizuri na ametoa tahadhari kwa wapinzani wao Bongo Movie kutarajia kadhia kubwa ya kupoteza mchezo huo muhimua mbao utaingia katika historia ya nchi ya Tanzania.

ANGALIA PICHA

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)


Post a Comment

0 Comments