Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.23,2016 SAA 05:18 USIKU
Ubingwa Kombe la CECAFA Chalenji kwa timu za mpira wa miguu za
wanawake katika nchi za Afrika Mashariki, umewavutia wadau
wengi kwa kiwango kikubwa hivyo kushusha neema kwa wachezaji hao wa timu ya taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Queens ambayo imeandika historia ya kutwaa taji hilo ikiwa ni taifa la kwanza katika mashindano hayo mapya.
wengi kwa kiwango kikubwa hivyo kushusha neema kwa wachezaji hao wa timu ya taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Queens ambayo imeandika historia ya kutwaa taji hilo ikiwa ni taifa la kwanza katika mashindano hayo mapya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,
amefurahishwa na ubingwa wa timu hiyo akisema: “Si ubingwa tu, bali
umefuta dhana ya Wakenya ambao siku zote wamekuwa wakitangaza Mlima
Kilimanjaro uko kwao Kenya wakati upo hapa Tanzania. Kwa kuifunga Kenya,
mmefanya kazi nzuri.”
Kutokana na ubingwa huo na kuitetea nchi, Nape ambaye aliongozana na
Wabunge sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliahidi
kuitafutia timu hiyo ya taifa ya wanawake mdhamini na kwa baadhi ya
wachezaji kupata ajira sehemu mbalimbali hususani kwa makampuni kadhaa
ambayo yamewekeza hapa nchini.
“Niko na Wabunge hapa. Bunge la Novemba ambalo litaanza Novemba mosi,
naawaalika bungeni. Tutazungumza na Spika ili kuvunja kanuni za bunge
iloi ninyi muingie bungeni la kombe letu. Nitawaomba wabunge wakate
posho zao kidogo, ili kuwazawadia ninyi pale mtakapofika. Tutakuwa na
mchezo wa mpira wa miguu kati yenu na wabunge, na kila bao moja
mtakalowafunga wabunge, litalipiwa Sh milioni moja.”
“Mimi ndiye nitakayehesabu mabao, lakini mkae mkijua haitakuwa kazi
rahisi kuwafunga wabunge. Wako vizuri,” alisema Nape ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Mtama na kauli yake hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti
wa Bunge Sports Club, William Ngeleja aliyeambatana wabunge wengine
akiwamo Makamu Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Esther Matiko.
Wengine waliokuwako ni Bupe Mwakang’ata, Alex Gashaza, John Kanuti
ambaye mbali ya ubunge pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kadhalika
Venance Mwamoto – nyota wa zamani wa timu ya Taifa na Kocha wa daraja B.
Kwa upande wa TFF, Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania, Jamal
Malinzi alitoa ahadi ya Dola za Marekani 10,000 (sawa na Sh milioni 22)
kwa timu hiyo baada ya kutwa taji hilo kabla ya timu hiyo leo kutembelea
Kampuni ya Airtel ambako Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel-Tanzania,
Beatrice Singano akatangaza kampuni yake kuendelea kudhamnini mashindano
ya kuibuka vipaji ambavyo vimekuwa vikiitoa Tanzania kimasomaso katika
mashindano ya kimataifa.
Kati ya nyota 20 wa Kilimanjaro Queens waliotwaa taji hilo, wanane
walipitia mashindano ya Airtel kwa miaka tofauti katika udhamini ambao
kwa mwaka huu ilikuwa ni mara ya sita kwa kampuni hiyo inayofanya vema
kwenye soko la huduma za simu, kudhamini mashindano ya Airtel Rising
Stars (ARS).
Safari ya ubingwa wa Kilimanjaro Queens ulianzia hatua ya makundi kwa
kuilaza Rwanda manbao 3-2 kabla ya kutoka sare tasa na Ethiopia ambayo
pia ilivuna ushindi wa mabao 3-2 kutoka kwa Rwanda. Tanzania na Ethiopia
zilitoka sare na kurusha sarafu ambako Tanzania ikawa ya kwanza katika
kundi B hivyo kucheza na Uganda ambayo ililala kwa mabao 4-0 katika
mchezo wa nusu fainali. Na leo Septemba 20, 2016 ikatawazwa kuwa
mabingwa kwa ushindi wa mabao 2-1.
Timu zote shiriki zilikuwa
Tanzania, Burundi, Zanzibar, Kenya, Ethiopia, Rwanda pamoja na mwenyeji
Uganda. Mashindano ya Kombe la Chalenji la CECAFA kwa timu za wanawake
yamefanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano
hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa nchi za Afrika
Mashariki na Kati.





0 Comments