Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.13,2016 SAA 11:21 JIONI
Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Azam FC na
Simba ya Dar es Salaam, utafanyika Jumamosi
Septemba 17, 2016 kama
ilivyopangwa awali.
Ila mchezo huo utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam badala ya
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa sababu za kuipa nafasi timu ya taifa
ya vijana ya mpira wa miguu ya Congo Brazzaville ambayo itakuwa nchini
kwa ajili ya mchezo wa ushindani dhidi ya wenyeji – Serengeti Boys
ambayo ni timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.
Timu hizo zinakutana kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo. Mchezo
huo utafanyika Septemba 18, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam
hivyo kutokana na kanuni za mashindano, siku moja kabla mgeni anapata
nafasi ya kufanya mazoezi.
Serengeti Boys ambayo ilipiga kambi Shelisheli kujiandaa na mchezo
huo ambako imejipanga vyema kuiondoa Congo Brazzaville katika michezo
miwili inayotarajiwa kuwa na ushindani mkali ukianzia huo wa Septemba
18, 2016 kabla ya kurudiana jijini Brazzaville hapo Septemba 30 au
Oktoba 1 au Oktoba 2, mwaka huu.
Mtendaji Mkuu wa (CEO) Azam FC, Saad Kawemba kwa mujibu wa kanuni ya 6
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kipengele cha 5 na 6, ameridhia
mchezo huo kufanyika Uwanja wa Uhuru hapo Septemba 17, 2016 na kufuta
upotoshwaji unaofanyika kwenye mitandao ya kijamiii.
Kawemba alizungumza hayo, mara baada ya kupokea Ngao ya Hisani halisi
mara baada ya tuzo hiyo kufika jijini Dar es Salaam ikitokea China
pamoja na vifaa vingine. Itakumbukwa kwamba awali Agosti 17, 2016 mara
baada ya kuishinda Young Africans kwa mikwaju ya penalti, Azam walipewa
Ngao ya mfano.
0 Comments