Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.SEPT.13,2016 SAA 11:22 JIONI
Timu ya Mpira wa Miguu ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya
miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imefanya kambi yake kwa
mafanikio huko jijini
Victoria kwenye Kisiwa cha Mahe, nchini Shelisheli baada ya kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya dhidi
ya Northern Dynamo.
Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa wa Shelisheli, bao
pekee la Serengeti Boys lilifungwa na Muhsin Makame katika dakika 75 ya
mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali katika vipindi vyote viwili
kutokana na kushambuliaana mara kwa mara.
Serengeti Boys ambayo ilikuwa na kikosi cha nyota 21 na viongozi
watano, wamemaliza kambi ya huko Shelisheli na hivyo inaondoka jioni ya
leo Septemba 13, 2016 saa 11:00 jioni na ikitarajiwa kuingia nchini
usiku wa saa 7:45 Septemba 14, 2016 ambako itakuwa kambini hadi siku ya
mchezo Jumapili Septemba 18, mwaka huu.
Mchezo huo wa kuwania kucheza fainali za kucheza fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Fainali
hizo zitafanyika jijini Antananarivo, Madagascar hapo Aprili, 2017.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Nyundo Shime maarufu kwa jina
la Mchawi Mweusi, amesema: “Sitaki kuwa na maneno mengi. Nataka
Watanzania waje kuona wenyewe. Maana maneno maneno yakizidi inakuwa kama
kero. Nataka kujenga utamaduni wa Watanzania kuja wenyewe uwanjani
kuona timu yao.”
Katika hatua nyingine, wapinzani wa Serengeti Boys wanatarajiwa kutua
Alhamisi wakiwa na kikosi cha watu 40 na kati ya hao ni 22 ni
wachezaji. Miongoni kwa kundi hilo pia kuna wanahabari wanne.
Katika orodha ilitumwa TFF, wachezaji wa timu hiyo ni pamoja na
Mathieu Lee Valtair, Balou Prince Joel, Bopoumela Chardon, Kiba Konde
Ridrique, Kibasila Christ Benilde, Langa Lessen Bercy, Makouana Beni,
Mantouari Juste Aldo, Mata Thomas, Mbemba Patchely Rael, Mbenza
Kamboleke, Mboungou Prestige, Mebeza Egouep Craiche, Mouandza Mapata,
Moungala Ikounga, Mountou Edouard, Ngakosso oko Alves, Ngaloukossi Jossy
Ronel, Nguienda Mouanga Bernice, Nguimbi Exau, Ntoto Gedeon, Oboua
Danish na Otang Jeordon.
Viongozi wa timu hiyo wamo Ntoto Lacombe ambaye ndiye Mkuu wa
Msafara, Goma Ambroise Stephane ambaye ni Mratibu wa msafara, Ngami
Gobard – Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Congo – Brazzavile.
Wengine ni maofisa mbalimbali Otende Charles, Moussavou Merrile,
Badji Mombo, Berrettini Paulo, Ekariki Basile, Cesana Eraldo, Bakoua
Loufouma Narcisse, Okandze Elenga Jean Pierre, Lounou Joste Feller,
Mabila Kengue Francois, Loemba Jean Rufin, Mendome Ndoum, Batangounna
Ntari na Mbemba Gervais.
0 Comments