Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:SWALA HILI HALITAKUWEPO KUEREKEA MECHI YA SERENGETI BOYS NA SHELISHELI

 Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 14,2016 SAA 02:01 USIKU 
Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Taifa ya vijana - Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys), Sebastian Nkoma na Mshauri wa Ufundi wa TFF kwa maendeleo ya timu za Vijana, Kim Poulsen wakisimamia mazoezi ya viungo kwa wachezaji wa kikosi hicho kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijiji Dar es Salaam leo Juni 15, 2016. Serengeti Boys ipo kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya vijana wenzao wa Shelisheli wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Juni 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. 
Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys), hii leo kimeanza mazoezi rasmi ya kujiandaa na mchezo wa
kuwani nafasi ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika kwa  vijana dhidi ya Shelisheli ambao umepangwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es salaam.

Kocha mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema vijana wote wapo katika hali nzuri na utaratibu wa mazoezi waliouandaa utakua unachukua nafasi yake asubihi na jioni katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Kocha mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime akiendesha mazoezi

SIKILIZA HAPA

HHata hivyo Shime ameendelea kuwaomba mashabiki wa soka nchini kuwa snjari ya kikosi chake ambacho kwa sasa ndicho kilichosalia katika majukumu ya kuitafutia nafasi Tanzania ya kucheza katika fainali kubwa za barani Afrika.
Shime ameongeza kwamba katika mchakato wa maandalizi ya kikosi hicho cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, hakutakua na mchezo wowote za kimataifa wa kirafiki zaidi ya kutumia mafunzo waliyoyapata kwenye michezo kadhaa waliyowahi kucheza ikiwepo ile waliyokwenda nchini India.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments