![]() |
| Wachezaji wa azam Fc wakishangilia bao (picha na Tanzaniatoday.co.tz) |
Waoka mikate Azam FC wametangaza msimami wao wa kuanza harakati za usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu mpya wa ligi
kuu ya soka Tanzania bara ambao umepangwa kuanza August mwaka huu.
Afisa habari wa Azam FC Jaffary Iddy Maganga amesema harakati za usajili wanatarajia kuzifanya mara tu, makocha wao kutoka nchini Hispania watakaporejea kutoka mapumzikoni huko nchini Hispania.
Hata hivyo Jaffary amesema usajili wao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi utazingatia sana wachezaji waliokuzwa katika kituo cha vijana cha Azam Complex kilichopo Chamazi jijini Dar es salaam.
SIKILIZA HAPA

0 Comments