Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:REFA WA 5 - 0 ZA SIMBA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA BAADA YA KUCHAGULIWA KUWA KIONGOZI WA YANGA...msikilize hapa..

  Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 14,2016 SAA 09:59 ALASIRI
Mwamuzi aliyechezesha mchezo  wa SIMBA 5 - 0 YANGA  , Hashim Abdallah, akimpa kadi ya njano aliyekuwa golikipa wa timu ya Yanga, Said Kasalama katika mchezo huo baada ya kumdondosha Emmanuel Okwi alipokuwa ndani ya eneo la penalti na kisha kupigiwa adhabu hiyo, iliyopigwa na marehemu Patrick Mafisango na kufanya Simba hadi wakati huo kuongoza kwa mabao 3-0.(Picha nwwwbayanablogspotcom.blogspot.com)

Siku chache mara baada ya kuchaguliwa kuingia katika kamati ya utendaji ya klabu ya Young Africans (Jumapili Jun
12,016) ,Mwamuzi mstaafu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, Hashim Mudhihir Abdallah,amefunguka katika mahojiano maalumu na Jamii na Michezo ,akielezea sababu za wanachama wa klabu hiyo kumuamini kwa kumpigia kura na hatimaye kumpa nafasi hiyo.
Mpaka dakika inayoonekana kwenye ubao wa matokeo, mabao yalikuwa kama inavyosomeka kwenye ubao huo.

 Hashim Mudhihir Abdallah ambaye alichezesha mtanange wa Simba na Young Africans uliomalizika kwa mnyama kuibuka na ushindi wa mabao matano kwa sifuri mwaka Mei 6, 2012, amesema wanachama wa klabu wa Yanga wana uelewa wa kutosha katika maswala ya michezo na ndiyo maana wakampa nafasi hiyo licha ya machungu ya mchezo huo.
Hashim Mudhihir Abdallah wa kwanza kushoto) akiwa na Wajumbe wengine wa kamati ya utendaji Yanga waliochaguliwa

Hashim ambaye amechaguliwa kwa kura 727,amesema kwa sasa anahisi ana deni kubwa la kuitumikia klabu ya Yanga,na ameahidi kupambana ili aweze kuleta furaha katika klabu hiyo.

MSIKILIZE HAPA
KKWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments