Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO: WAKILI WA TFF ATOA SABABU ZA KUJITOA KUSIMAMIA UCHAGUZI WA YANGA..msikilize hapa...

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 3,2016 SAA 01:05 USIKU
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF, Aloyce Komba akizungumza leo
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF, Aloyce Komba ametangaza kujiweka pembeni katika
mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Young Africans kufutia jina lake kutajwa katika sauti zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii, zikihusishwa na mpango wa kuvuruga uchaguzi wa klabu hiyo.

Komba amesema haoni uzito wayeye binafsi kuendelea kuwepo katika mchakato huo, ikiwa tayari jina lake limehusishwa katika tuhuma za kuvuruga kwa makusudi uchaguzi.

Hata hivyo Komba ametoa sababu mbalimbalia mbazo zinamfanya kujiengua katika shughuli za kuratibu uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na maneno mazito yaliyozungumzwa na mwenyekiti wa young Africans Yusuf Manji.

MSIKILIZE HAPA
AAloyce komba pia amemuomba rais wa TFF kukasimisha madaraka yake kwa makamu mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini.
Katika hatua nyingine Komba amesema kwamba hazitambui sauti ambazo zinazungumzwa kwenye sautiz zilizowekwa hadharani na mwenyekiti Yusuph Manji na anashangaa kwa nini sauti hizo ziweza kumuhusisha yeye ili hali hausiki chochote na mpango huo.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments