Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:MANJI ACHUKUWA FOMU YA KUTETEA NAFASI YAKE YANGA SC

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 2,2016 SAA 11:51 JIONI
Mwenyekiti wa klabu bingwa Tanzania bara, Young Africans Yusuf Manji amelituhumu wazi wazi shirikisho la soka nchini TFF kwa
kusema limekua chanzo cha kuleta vurugu ndani ya klabu hiyo.

Manji ambaye hii leo amechukua fomu za kutetea nafasi ya uenyekiti wa klabu hiyo, amesema TFF imekua mstari wa mbele kuihujumu Young Africans na haikutosheka na mpango huo na badala yake imejiingia katika suala la kutaka kusimamia uchaguzi.

Amesema kwa kiasi kikubwa TFF imekua ikifanya hivyo kwa lengo la kumuondoa madarakani yeye kama mwenyekiti ambay kwa kipindi kirefu ameonyesha kuziba mianya ya kuizorotesha Young Africans kimaendeleo.




Manji hakuishia hapo bali alikwenda mbali zaidi na kufichua fumbo ambalo lilifumbwa jana na mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Young Africans, Jerry Muro kwa kusema kuna baadhi ya watu wamekua wakifanya makusudi ya kuvuruga uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.

Manji amethibitisha kuwa na sauti zinazodhaniwa kuwa za viongozi wa TFF, BMT pamoja na baadhi ya wanachama na ameagiza suala hilo kufikishwa katika vyombo vya usalama kwa uchunguzi zaidi.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments