Ticker

6/recent/ticker-posts

AUDIO:MKWASA AZUNGUMZIA MFUMO WA KUIANGAMIZA MISRI,KUMKOSA KANAVARO NA WACHAMBUZI WA KIBONGO

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 3,2016 SAA 01:40 USIKU
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, charles Boniface Mkwasa akizungumza leo
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, charles Boniface Mkwasa ameahidi kutumia mfumo wa kushambulia zaidi katika
mchezo wa kesho ambao utashushudia Taifa Stars wakipambana na mabingwa wa kihistoria barani Afrika timu ya taifa ya Misri.

Mkwasa amesema dhumuni kubwa la kutarajia kutumia mfumo huo, ni kutaka kuwapa changamoto wapinzani wao Misri ambao kwa hakika kesho watakua wanahitaji sare ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwenye fainali za Afrika za mwaka 2017, ambazo zitachezwa nchini Gabon.

Amesema pamoja na kutarajia mfumo huo kama ngao kubwa ya Stars kusaka point tatu muhimu, bado wanawaheshimu Misri kama timu bora na yenye kiwango kikubwa kuliko tanzania, lakini bado akaendelea kusisitiza suala la kuzitumia vyema dakika 90 za mchezo wa kesho.

MSIKILIZE HAPA

HHata hivyo Mkwasa ametoa ushari wa bure kwa wachambuzi wa soka nchini, kwa kutoa nafasi kwa timu yake kucheza kwanza mchezo wa kesho na ndipo watoe mtazamo wao, ili kuepusha hali ya kuwavunja moyo wachezaji wake kama watachukua jukumu la kuwasilisha maoni yao kabla ya kipyenga hakijapulizwa hiyo kesho kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Wakati huo huo Mkwasa, amekataa kata kata kuzungumzia suala la mchezo mmoja mmoja baada ya kutakiwa kueleza mipango yake kufutia wito wake kwa Narid Haroub Canavaro kukwama tangu walipokua wakielekea nchini kenya kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafikia mbao ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) . 

Post a Comment

0 Comments