Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa klabu ya Young Africans Jerry Muro, hii leo amewasilisha rasmi barua pamoja na
vielelezo vya hujuma za kuvuruga uchaguzi mkuu wa klabu hiyo katika ofisi za taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU.
vielelezo vya hujuma za kuvuruga uchaguzi mkuu wa klabu hiyo katika ofisi za taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU.
Muro amewasilisha barua pamoja na vielelezo hivyo ikiwa ni kutii agizo alilopewa na mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Yusuf Manji mwishoni mwa juma lililopita, dakika chache kabla ya kuchukua fomu za kutetea nafasi yake.
Muro amesema wanaamini TAKUKURU itatenda haki na kufikia hatua ya kuwabaini wahusika kwa kutumia vielelezo na kufikia hatua ya kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Naye Afisa habri wa TAKUKURU, Mussa Msalaba amethibitisha kupokelewa kwa barua pamoja na vielelezo vya hujuma za kuvuruga uchaguzi mkuu wa young Africans, na kuahidi yatafanyiwa kazi kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria za nchi.
SIKILIZA HAPA
SIKILIZA HAPA

0 Comments