Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam umesema kuwa umepokea kwa furaha kubwa usajili wa Mbwana Ally
Samatta ambaye amejiunga na klabu ya Genk ya nchini Ubeligiji akitokea katika klabu ya tp mazembe.
Samatta ambaye amejiunga na klabu ya Genk ya nchini Ubeligiji akitokea katika klabu ya tp mazembe.
Hayo yamesemwa na mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo ya simba Saidy Tuli wakati akizungumza na kipindi hiki,
Samatta alijiunga na Mazembe mwaka 2011 kwa dau la Sh. Milioni 100,000 akitokea Simba SC na juzi ametambulishwa rasmi kujiunga na klabu hiyo ya Koninklijke Racing Club Genk kwa Mkataba wa miaka minne na nusu.
Saidi Tully amesema Watanzania wangi walikuwa wanategemea mengi kutoka kwa mchezaji huyo na anaamini mchezaji huyo atafungua njia kwa wachezaji wengine.
MSIKILIZIZE SAID TULLY
JSaid Tully pia amesema Klabu ya simba inaamini kuwa kila kitu kikiwa kimekamilika klabu ya Tp Mazembe itaweza kuwagawia mgao wao kutoka klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutokana na mauzo ya mshambuliaji Mbwana Ally Samatta.
Katika hatua nyingine Said Tully amesema wiki ijayo katibu mkuu wa Simba, ataweza kufanya mawasiliano na Tp Mazembe kuona kuwa wanapata mgao wa aslimia 20 ,ambapo klabu ya simba inategemea kupata mgawo wao wa Euro 160,000 kutoka klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutokana na mauzo ya mshambuliaji Mbwana Ally Samatta.
ANGALIA VIDEO SAMATTA AKITAMBULISHWA
Mjumbe huyo wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo ya simba Saidy Tully pia hakusita kutoa wito kwa vijana wa mchezo wa soka hapa nchini,kuweza kufuata nyayo za Mbwana Ally Samatta.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments