|
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limesema hakuna vita kati ya Shirikisho na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA)
bali mawasiliano yanaendelea kati ya TFF na vyombo husika kuhakikisha ZFA ambaye ni mwanachama mshiriki wa CAF anaendesha shughuli zake kwa mujibu wa taratibu.
bali mawasiliano yanaendelea kati ya TFF na vyombo husika kuhakikisha ZFA ambaye ni mwanachama mshiriki wa CAF anaendesha shughuli zake kwa mujibu wa taratibu.
Kanuni na taratibu za CAF ziko wazi kuhusu nani aongoze Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na anapatikana kwa utaratibu upi.
Kikubwa ni kuzuia ZFA isipate madhara ya kufungiwa na Chama Cha Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Theophil Makunga kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) mwishoni mwa wiki.
Katika salamu hizo, Malinzi amempongeza Makunga kwa nafasi hiyo aliochaguliwa na kusema imani waliyonayo wahariri wenzake juu ya utendaji wake wa kazi ndio kumepelekea wao kumchagua kuongoza jukwa hilo.
Aidha Malinzi amewapongeza Deodatus Balile aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti na Neville Meena aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa hilo na kuahidi kuwa TFF itaendelea kushirikiana nao.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments