Ticker

6/recent/ticker-posts

BAADA YA SAMATTA KUJIUNGA NA GENK,HIKI NDICHO KILICHOKISEMWA NA TFF

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jan.30,2016 SAA 08:34 MCHANA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa timu ya Taifa ya
Tanzania “Taifa Stars” Mbwana Samatta kwa kufanikiwa kujiunga na klabu ya Racing Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ubeligiji.
Malinzi amempongeza Samatta kwa kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Ubeligiji baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kuichezea RC Genk inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo.
Kufuatia kupata nafasi hiyo, Malinzi amemtaka Samatta kujituma kwa nguvu zake zote na uwezo wake wote ili kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika nyanja za kimataifa na kwa sasa barani Ulaya.
Aidha Malinzi amewataka wachezaji wengine kujituma na kutumia nafasi wanazozipata katika vilabu vyao kwa kufanya vizuri na kupata nafasi ya kuvuka kwenda kucheza soka la kimataifa nchi za nje.
SWAI KUZIKWA LEO KNCU - SAWE
Aliyekua Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu, Epaphra Swai anatarajiwa kuzikwa leo jioni saa 10 katika kijiji cha Sawe, Masama Mashariki.
Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu itafanyika leo Jumamosi saa 9 alasiri, kitongoji cha Ituuny kijiji cha Sawe, na mazishi yake yatafanyika katika eneo la KNCU kata ya Masama Mashariki.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linaendelea kutoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki, wadau wa mpira wa miguu pamoja na familia ya marehemu, katika kipindi hiki kigumu cha maombelezo ya msiba huo.
Marehemu Epaphra Swai aliaga dunia Alhamisi asubuhi katika hospital ya taifa ya Muhimbili.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments