Ticker

6/recent/ticker-posts

TAARIFA JUU YA KOCHA MPYA WA MAZOEZI YA VIUNGO KUSAINI MKATABA RASMI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.02,2015 SAA 01:15 USIKU
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva akibadilishana mkataba na kocha mpya wa mazoezi ya viungo Dušan Momčilović
Kocha huyo kutoka Nchini Serbia ana uzoefu mkubwa katika fani ya mpira wa miguu hususani mazoezi ya
viungo.
 Kocha Dušan amefundisha klabu mbalimbali duniani kwenye Nchi kama Malaysia, Indonesia, Georgia ambako Alikuwa kocha wa mazoezi ya viungo wa klabu ya FC DINAMO ambayo ilicheza mechi za awali ya klabu bingwa ya Ulaya-UEFA, Bosnia and Herzegovina, Oman na Belgrade
Kocha Dušan pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu ya FC SOGOR –Tobruk – Libya.
Kocha Dušan ni muhitimu wa Digrii ya Mazoezi ya Viungo jijini Belgrade akiwa amejikita Zaidi kwenye mazoezi ya viungo na kujenga mwili.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments