Ticker

6/recent/ticker-posts

RAHEEM STERLING AKOSA MAZOEZI NA LIVERPOOL KWA SIKU YA PILI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.09,2015 SAA 10:37 JIONI

Raheem Sterling amekosa kuhudhulia tena mazoezi baada ya kutoa taarifa ya ugonjwa kwa siku ya pili hii leo.


Chombo cha Sky Sports News kiliambiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kuwa anataka kuondoka katika klabu ya Liverpool kwa sababu ya maswala ya meneja Brendan Rodgers -pamoja na kwamba chanzo cha karibu katika klabu hiyo, alikana vikali madai hayo.

Sterling ameomba kuachwa nje ya kikosi kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu kwa Liverpool ambapo wataondoka Mashariki ya Mbali na Australia siku ya Jumapili.

Liverpool tayari wamekataa ofa mbili - pamoja na ya £ 40m - kutoka Manchester City kwa ajili Sterling na Rodgers bado nia ya kuwa na mchezaji huyo.
Sterling bado ana mkataba na Liverpool mpaka 2017, lakini uhusiano wake na klabu ya Liverpool umeshuka tangu apige chini nafasi ya kutia saini mkataba ulioboreshwa mwezi Januari.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments