Ticker

6/recent/ticker-posts

KAGAME CUP:YANGA YACHAPWA NA GOR MAHIA,KMKM YATOKA KIMASOMASO,APR JE?(PICHA NA MATOKEO)

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.JULY.18,2015 SAA 02:00 USIKU 


Michuano ya Kagame imeanza kupamba moto kwa vilabu mbalimbali kucheza mechi za kwanza katika viwanja vya
karume na Taifa jijini Dar es salaam,vikiwa na lengo la kusaka Ubingwa wa michuano hiyo.

Katika mchezo wa kwanza APR ya Rwanda ilimeanza vyema michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati  kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Shandy ya Sudan katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo mwingine Yanga SC, leo imeanza vibaya michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi cha Gor Mahia

Kikosi cha Yanga














Kocha mkuu wa Gor Mahia Frank Nuttal 


Yanga walitangulia kupata bao katika dakika ya 5 tu ya kipindi cha kwanza baada ya Gor Mahia kujifunga baada ya krosi iliyochongwa na Donald Ngoma.


Dakika ya 16 ya mchezo huo Harun Shakava wa Gor Mahia akasawazisha kwa kichwa.

Katika Dakika ya 24, Ngoma alipewa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kufuatia kumsukuma Shakava baada ya kumpamia na mpira hadi nje ya Uwanja .

Mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika kipindi cha kwanza.
(Juu na Chini)shabiki wa Yanga anayejulikana kama Ally Yanga akiwa ameshika viungo vya mboga



Donald Ngoma na wachezaji wenzake wakishangilia bao la Kuongoza
















Gol Mahia Wakienda mapumziko kupitia mlango tofauti na Yanga


Kipindi cha pili, Gor Mahia waliingia na mashambulizi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya kwanza tu kupitia kwa mshambuliaji wake, Michael Olunga

















Yanga SC walipoteza nafasi nzuri ya kupata ya bao la kusawazisha baada ya Nahodha Nadir Haroub Cannavaro kupiga mkwaju wa penalty iliodakwa na  kipa Oluoch wa Gor Mahia.

Dakika tano za mwisho za kipindi cha pili Yanga walicharuka na wachezaji wote kupanda mbele kulishambulia lango la Gor Mahia,lakini matokeo yakabaki vile vile,Yanga 1 - 2 Gor Mahia.


Na mchezo mwingine ulipigwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam,kati ya KMKM  na Telecom(DJB),na KMKM kuchomoka na ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya Telecom.






KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments