![]() |
| Ofisa habari wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Temeke (katikati)Ben Mwanantala akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kulia ni katibu mkuu wa chama hiko Hassan Mustapha |
Chama cha mpira wa miguu wilaya ya Temeke (TEFA) hii leo Kimetangaza kuanza rasmi mchaakato wa uchaguzi wa chama hiko
utakaofanyika tarehe 16 mwezi wa nane mwaka huu.
utakaofanyika tarehe 16 mwezi wa nane mwaka huu.
![]() |
| kikao cha kamati ya utendaji kikiendelea |
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo katibu mkuu wa chama hiko Hassan Mustapha amesema,mara baada ya kufanyika kwa kikao cha kamati ya utendaji,wameamua zoezi rasmi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi katika chama hiko,litakuwa rasmi tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka huu.
Katika hatua nyingine Hassan Mustapha amemtangaza Ofisa Habari wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Temeke (TEFA) ambaye ni Ben Mwanantala.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kama ofisa habari wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Temeke (TEFA)Ben Mwana ntala amekishukuru chama hiko kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo.
MSIKILIZE KATIBU WA TEFA HASSAN MUSTAFA NA BEN MWANANTALA
RATIBA YA MATUKIO YA UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA TEMEKE
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)





0 Comments