Klabu ya Simba hii leo imetangaza kuimeingia mkataba wa mwaka mmoja na Dylan Kerr kama kocha mpya na anatarajiwa kuanza
kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi July.
Akimtangaza kocha huyo,raisi wa klabu ya Simba Evansi Aveva amesema kuwa Kocha huyo kutoka Nchini Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.
Kocha Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na South Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini
Aveva ameongeza kuwa Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha huyu mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, na wana amini atakuwa chachu ya mafanikio pia kwa kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba.
Kerr ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.
Kwa taarifa zaidi za wasifu wa Kocha Dylan Kerr fuata Link hizi...http://simbasports.co.tz/wp-content/uploads/2015/06/SIMBA-SPORTS-CLUB-DYLAN-KERR-CV.pdf
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)
0 Comments