Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:TAIFA STARS YAFUNGWA NA MISRI

Mhariri:Herman Kihwili. IMEWEKWA.Jun 15,2015 SAA 01:10 USIKU
Displaying Ulimwengu akiwania mpira na mlinzi wa Mirsi.jpg
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imepoteza mchezo
wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 - 0 na wenyeji Misri.

Taifa Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 - 0.
Displaying Kikosi cha Taifa Stars.jpg
Displaying Balozi wa Tazania, Mh. Mohamed Hamza (mwenye tai nyekundu) akiimba wimbo wa taifa.jpg
Displaying Baadhi ya watanzania walipata nafasi ya kushuduia mchezo.jpg
Displaying Ulimwengu akiwania mpira na mlinzi wa Mirsi.jpg

Kipindi cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3 ndani ya dakika 10, kupitia kwa Ramy Rabia(60), Basem Morsy(64) na Mohamed Salah (69). 

Stars ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim Mbdonde na kufanya shambulizi kadhaa langoni kwa Misri lakini mashambulzi hayo yaliokolewa na walinzi wa timu ya Misri.

Mara baada ya mchezo huo, Taifa Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea Cairo ambapo itaondoka na shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na kufika jijini Dar es salaam jumanne saa 7 mchana.

Tanzania: Deogratias Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim Mbonde, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Amri Kiemba/Frank Domayo.

Misri: Ahmed El Shenawy, Ahmed Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy, Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan Meky.

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo)

Post a Comment

0 Comments