Ticker

6/recent/ticker-posts

PICHA:TANZANIA YAICHAPA TENA KENYA BEACH SOCCER

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Feb.21,2015 SAA 01:46 USIKU
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) hii leo imechomoka na ushindi wa mabao 7 kwa 6
katika mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, mchezo uliopigwa jioni ya leo katika fukwe za Escape One Club Msasani jijini Dar es salaam.

Katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mombasa, timu ya Taifa ya Tanzania iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 3 dhidi ya wenyeji timu ya Taifa ya Kenya na kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Tanzania sasa imefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 12  kwa 9 ya Kenya.

Fainali za Soka la Ufukweni zinatarajiwa kufanayika mapema mwaka huu katika Visiwa vya Shelisheli.

Picha zote na page ya Facebook ya Tff

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments