Manuel Pellegrini ana amini kuwa Manchester City wanaweza kukabiliana,hata bila kuwa na mchezaji Yaya
Toure katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona.
kiungo huyo hatakuwepo kwa mechi ya kwanza ya City hatua ya -16 mchezo dhidi ya Timu ya Barca ya Hispania usiku wa leo Jumanne, lakini wachezaji wenzake wilifanya vizuri katika michezo miwili ya awali ambayo mchezaji huyo hakuwepo poa, kwa kushinda mabao 3-2 dhidi ya Bayern Munich na mabao 2-0 dhidi ya Roma na kujitanua katika nafasi yao ya hatua ya mtoano.
Toure alirejea City baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika na kucheza kwa dakika 90 siku ya Jumamosi jioni na City ikashinda kwa mabao 5-0 dhidi ya Newcastle United.
Na Manuel Pellegrini anakubali kuwa nyota huyo wa Ivory Coast ni mchezaji muhimu kwa yake, lakini anahisi timu yake inaweza kubeba jukumu lake dhidi ya Barcelona ambayo ameshinda michezo 11 mfululizo kabla ya kufungwa kwa bao 1-0 na Malaga hivi karibuni katika La Liga mwishoni mwa wiki.
"daima napendelea kucheza na Yaya,ni mchezaji muhimu sana na sisi daima tucheza vizuri na Yaya," alisema meneja City.
"Lakini tunawezi kufanya vizuri bila yeye, kwa sababu sisi tulifanya vizuri dhidi ya Bayern na Roma na tuna kikosi kizuri cha kuziba nafasi yake."
City walipigwa 2-0 nyumbani na Barcelona katika hatua kama hii ya msimu uliopita na pia walipoteza mechi ya pili katika dimba la Nou Camp, kwa kufungwa 2-1.
Lakini Pellegrini anasema timu yake itakuwa bora kwani wachezaji wake wamekuwa wazuri, kwa sababu ya ratiba hii imewajenga kimchezo,kwani wamekuwa wakicheza michezo mingi, lakini pia akisisitiza kwamba,ni lazima timu yake itambue kwamba wanakwenda kucheza dhidi ya timu imara sana,yenye vipaji mbalimbali.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments