Arsene Wenger ana wivu wamafanikio kama mameneja wote duniani , kwa sababu ana "Ndoto kazi" kwa Arsenal, hayo
yamesemwa na kukumbushwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho.
Wenger imekuwa Kiongozi wa Arsenal tangu mwaka 1996, ameshinda mara tatu taji la Ligi Kuu, mara tano Kombe la FA na kusimamia hoja ya kuondoka katika dimba la Emirates.
Mfaransa huyo hatimaye alitwaa Kombe la FA mwaka jana,baada ya ukame wa makombe kwa miaka tisa-Lakini licha ya shinikizo kutoka kwa mashabiki wakitaka ajiuzulu, bodi ya Arsenal bado wanaonekana waaminifu kwa Wenger.
Mourinho, ambaye amekuwa akitupiana maneno mara kadhaa na Wenger katika siku za nyuma, anaamini mpinzani wake anastahili kuwa na furaha - lakini akamuonya kuwa kikosi chake kina vipaji na lazima akae mkao wa kuliwa tena hivi karibuni.
"Nadhani kila meneja ulimwenguni angependa kuwa na utulivu kwa kuwa hapa, baada ya mwaka na mwaka, kununua, kuuza na kujenga na kusubiri na kusubiri wee!,kwa ajili ya mafanikio.
"Alichokifanya kwa kushinda vikombe hivyo vengi katika kipindi fulani, ikampa uaminifu , yeye anastahili".
" ni meneja mzuri lakini nadhani ana hali nzuri ya kuwa na mafanikio. Wakati naangalia wachezaji na kikosi chake, kweli mimi nadhani atashinda. "
Jose Mourinho anasema yeye haelewi kwa nini Arsenal wamekuwa hawana mafanikio makubwa kwa miaka ya hivi karibuni ikiwa timu hiyo ina kikosi chenye vipaji
Lakini katika hatua nyingine Mourinho pia amesema anamuunga mkono Louis van Gaal kwa kujiunga na Manchester United licha ya kocha huyo kuanza kwa maisha magumu katika dimba la Old Trafford.
Bosi huyo wa zamani Real Madrid, ambaye alifanya kazi na van Gaal katika klabu ya Barcelona kama msaidizi wake wa zamani wa mchezaji,na anaamini kocha huyo anahitaji muda wa kukabiliana na maisha katika Ligi Kuu.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments