Ticker

6/recent/ticker-posts

KUELEKEA MCHEZO WA LEO, BEKI WA BARCELONA GERARD PIQUE AMEYASEMA HAYA KUHUSU YAYA TOURE NA WAPINZANI WAKE WA ZAMANI MANCHESTER CITY

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Feb.24,2015 SAA 09:48 USIKU
Beki wa Barcelona  Gerard Pique anasema kwamba anadhani Manchester City ni moja ya timu za juu
katika dunia na wanaweza kuwa mabingwa wa ligi ya mabingwa ulaya hapo baadaye.

Hata hivyo, Pique anadhani kukosekana kwa kiungo menye ushawishi wa City ,Yaya Toure kunaweza kuwa sababu ya kupoteza mchezo siku ya leo Jumanne usiku katika uwanja wa Etihad .
Barca iliwapiga City kwa matokeo ya jumla ya mabao 4-1  katika hatu ya mwisho ya-16 bora ya Ligi ya Mabinga  msimu uliopita na Timu hizo zinakutana kwa mara nyingine tena muda huu.

Na, akizungumza Kuelekea mchezo huo wa kwanza,Gerard Pique  aliyekuwa Kuichezea Manchester United, alikiri kwamba amevutiwa na yale aliyoyaona kutoka katika kikosi cha City katika Ligi Kuu England.
"Katika Premier League wao wanaonesha ni moja ya timu bora duniani," alisema.
"Natumaini katika miaka ijayo watapigana kwa ajili ya shindano hili - lakini si mwaka huu!"
City watakuwa bila Nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Toure katika mechi hii ya leo Jumanne na Pique aliongeza: "Yeye ni Mchezaji muhimu sana,sana kwa ajili ya kikosi cha City,akisisitiza kuwa anapokuwepo Yaya Toure na asipokuwepo kunakuwa na tofauti.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments