Ticker

6/recent/ticker-posts

JUAN MATA ANASEMA MANCHESTER UNITED ITARUDI LIGI YA MABINGWA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Feb.24,2015 SAA 10:23 ALFAJIRI
Juan Mata anasema ni muhimu kwa Manchester United kurudi tena na kucheza Ligi ya Mabingwa katika dimba la Old
Trafford msimu ujao.

United wamepoteza mchezo siku ya jumamosi kwa kupigwa 2-1 na Swansea , lakini Mata bado ana ana imani na msimu huu unaoelekea mwishoni.

Man United chini ya kocha Louis van Gaal watakutana na Sunderland na Newcastle katika michezo miwili ya Ligi kuu kabla ya kucheza katika robo fainali ya Kombe la FA na Arsenal Machi 9, na wakifuatiwa na mechi mbili kubwa dhidi ya Spurs katika Dimba la Old Trafford na Liverpool katika uwanja wa Anfield.

Akizungumza na Sky Sports News  Juu ya mfuko wa kusaidia watu wa Manchester United  katika shule ya Swinton, Mata alisema: " bado kuna michezo mingi ya kwenda kucheza,tuko katika mbio za kushinda Kombe la FA,kwa hiyo tutajaribu kushinda kwa sababu ni muda mrefu tangu klabu ishinde na ni muhimu sana kwetu kushinda"
Juan Mata Fred the Red, booked. Nice day with @manchesterunitedfoundation at The Swinton High School!
Fred the Red, booked. Nice day with @manchesterunitedfoundation at The Swinton High School!

"Ni wazi kwamba ni muhimu kwetu kuwa ndani ya nafasi nne za juu mwishoni mwa msimu wa ligi".
"Hivi sasa,Tunakabiliwa na wakati muhimu katika Ligi Kuu. Ni wazi mechi 10 za mwisho ni muhimu sana na pia tuna Kombe la FA dhidi ya Arsenal. Itakuwa ni vigumu lakini nadhani tutafanya hivyo kwa sababu ni wakati muhimu na inabidi kucheza"alisema Juan Mata
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments