Beki wa Paris Saint-Germain David Luiz anasema anatarajia upinzani mgumu wakati timu yake hiyo itakapokutana na
klabu yake ya zamani ya Chelsea katika Ligi ya Mabingwa siku ya leo Jumanne.
Luiz aliondoka Stamford Bridge na kutua Parc de Princes kwa ada ya uhamisho £ 50 msimu uliopita na mchezaji huyo anasema anaamini kuwa Chelsea imewekeza fedha vizuri.
Ada iliyopokelewa kwa ajili Luiz ilimsaidia bosi wa Chelsea Jose Mourinho kumleta Diego Costa, Cesc Fabregas na Filipe Luis nyota wa kimataifa wa Brazil,na Luiz anaamini kikosi cha Mourinho kina nguvu kwa sababu ya wachezaji walioongezeka.
David Luiz anasema kuwa anaamini pia PSG itakuwa klabu bingwa miaka si mingi,kwani kila siku klabu hiyo imekuwa na maendeleo.
0 Comments