Jose Mourinho amewaahidi mashabiki wa Paris Saint-Germain kwamba wataiona tofauti timu yake ya Chelsea na
si kama vile walivyopoteza kwa mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa katika dimba la klabu hiyo Parc des Princes msimu uliopita.
David Luiz aliyeondoka Chelsea na kujiunga PSG kwa ada ya uhamisho £ 50 msimu uliopita, aliiongoza Chelsea katika Mchezo wa kwanza uliomalizika kwa Chelsea kufungwa 3-1 na Paris, kabla ya kushinda katika mechi ya pili mabao 2-0.
David Luiz amedai Chelsea ni timu bora tangu alipoondoka, lakini Mourinho alikataa kutoa maoni juu ya David Luiz kuisaidia timu yake akisema kuwa hayuko tayari kuwazungumzia wapenzani,huku pia akiweka bayana ujio wa Diego Costa
"siko hapa kutoa maoni kuhusu wapinzani nasema, hata kwa David.sitaki kutoa maoni," alisema.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amethibitisha kuwa mshambuliaji Diego Costa ataanza katika mchezo wao wa leo wa Ligi ya Mabingwa wa raundi ya 16 dhidi ya Paris Saint-Germain.
Costa alikosa mechi tatu kubwa za ndani baada ya kufanya ubabe katika mechi dhidi ya Liverpool katika nusu fainali ya Kombe la Capital One.
Mourinho amewasha taa za kijani kwa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania licha ya awali kukiri juu ya wasiwasi wa kumchezesha moja kwa moja katika mechi hiyo muhimu.
"Ndiyo, nitamwanzisha. Lakini sidhani ni nzuri kwa mchezaji kuwa na wiki tatu au mechi tatu bila kuanza mchezo," hivyo sidhani yeye kama atakuwa bora kwa hali yake, "alisema Mreno huyo.
MECHI ZA LEO
MECHI ZA LEO
22:45
22:45
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments