Ticker

6/recent/ticker-posts

ADNAN JANUZAJ ALIA NA MFUMO WA LOUIS VAN GAAL,ATAJA NAFASI ANAYOTAKA KUPAGWA

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Feb.04,2015 SAA 11:55 JIONI
Adnan Januzaj amekubali kuwa mfumo wa Louis van Gaal anaoutumia katika klabu ya Manchester United umekuwa
'mgumu zaidi kwake kucheza'.

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji amekuwa na wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza msimu huu chini  Mholanzi huyo, na amechezeshwa katika nafasi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kama  wing-back katika mfumo wa 3-5-2.

Msimu uliopita chini ya kocha David Moyes mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19  alikuwa na mchango muhimu kama  winga mshambuliaji  au mshambuliaji, na alikuwa  katika nafasi nzuri.

Amekuwa akitajwa kuwa ataaondoka msimu huu lakini  Januzaj ameulizwa kwamba anaona kuwa anakatishwa tamaa zaidi?.

"Ndiyo, mfumo unaweza kufanya kuwa ngumu zaidi kwangu na kucheza,lakini ninafanya kazi," Januzaj alisema.

"nafanya mazoezi kila siku, nataka kupata michezo zaidi msimu huu".

"Najisikia si wing-back . Ni vigumu kwangu kwa sababu nahusika kulinda zaidi na mimi si mlinzi wa kweli. "
Pamoja na Januzaj kusisitiza msimamo wake wa kuwa mshambuliaji zaidi, baada ya kuanza kwa kucheza mechi tano tu za ligi chini ya Van Gaal, anajua kuwa anaweza kuwa na kuchukua nafasi yake popote yeye atakapowekwa kucheza.
" inategemea jinsi mchezo wangu utakavyokuwa," Januzaj aliongeza.
"Nafasi yangu maalumu ni kama No 10 au winga".alifafanua
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments