TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SHOMARI KAPOMBE
SIMBA SC
imepokea rasmi barua kutoka Azam FC inayoeleza kwamba imekubaliana na klabu ya
AS Cannes kumnunua mchezaji
Shomari Kapombe aliyewahi kuichezea Simba.
Katika barua
hiyo, Azam FC imeeleza kwamba gharama za uhamisho huo ni kiasi cha Euro 43,000
na kwamba Simba SC inatakiwa kupewa asilimia 40 ya kiwango hicho.
Simba SC
inapenda kuutangazia umma kwamba tayari imepata ushahidi unaoonyesha kwamba
kiwango kilicholipwa kwa ajili ya mchezaji huyo ni zaidi ya hicho kilichotajwa
na Azam FC.
Kwa sababu
hiyo, Simba SC jana imepeleka barua kwa klabu ya AS Cannes kupitia kwa Katibu
Mkuu wake, Xavier Nielsen, ikiomba mwongozo kuhusu utata huu uliojitokeza ambao
haukutakiwa kuwepo.
Kimkataba,
Simba SC inatakiwa kulipwa asilimia yake ya mgawo na CANNES na si timu ambayo
imemnunua Kapombe.
Simba SC ina
matumaini kwamba suala hili litafika mwisho wake kabla ya kufunguliwa kwa
Dirisha la Uhamisho wa Wachezaji Juni 15 mwaka huu.
Uongozi wa
Simba SC unaomba wapenzi na wanachama wake kutotaka kulitumia suala la Kapombe
kama sehemu ya kampeni za uchaguzi katika wakati huu na badala yake kutumia
busara ya hali ya juu kuhakikisha klabu inapata haki zake zote kwenye suala
hili.
Hakukuwa na
kuchafuana wakati wa mauzo ya Mbwana Samatta, Patrick Ochan, Emmanuel Okwi na
Mwinyi Kazimoto na ni matumaini ya uongozi kwamba hakutakuwa na tabia za
kutoaminiana wakati mazungumzo kuhusu uhamisho wa Kapombe yakiendelea.
Kama
ilivyokuwa kwenye mauzo mengine ya wachezaji ambayo yamefanywa na uongozi huu,
suala la Kapombe litakapokamilika, taarifa itatolewa kwa umma na hakutakuwa na
usiri wa aina au namna yoyote.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Katibu Mkuu
Simba SC
0 Comments