Mashindano ya mchzo wa Chess kati ya timu ya Tanzania na Kenya yamemalizika hii leo kwa fainali iliyopigwa katika Ukumbi wa Golden Jubilee Towers uliopo jijini Dar es salaam,ambapo timu
kutoka kenya imefanikiwa kuibuka na ushindi.
Mashindano hayo yaliyoanza tarehe 5,yalihusisha timu ya Tanzania ambayo ilikuwa na wachezaji kumi na timu ya Kenya nayo ilikuwa na wachezaji kumi, na Kenya kuwa washindi baada ya kuwa na alama nyingi.
Abel Magana kutoka Kenya ndiye aliyekuwa na alama nyingi zaidi,akifuatiwa na Mtanzania Geoffrey Mwanyika.
Lengo kubwa la mashindano hayo kwa timu ya Tanzania ni kuweza kupata viwango vya juu (Ranking) vya shirikisho la mchezo wa Chess duniani, lililoko Ugirika,ili Tanzania iweze kupata nafasi za kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI
Abel Magana kutoka Kenya (kulia) akikabiziwa kikombe |
Kushoto ni Geoffrey Mwanyika akikabiziwa kikombe |
ZIFUATAZO NI PICHA ZA WASHIRIKI KWA UJUMLA WAKIVALISHWA MEDALI
0 Comments