Mgombea urais Prince Ali Bin Al Hussein ametoa wito wa kusitishwa kwa "utamaduni wa vitisho" ndani ya FIFA.
Bosi huyo wa Jordan FA,na makamu wa rais wa FIFA pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya shirikasho, ni miongoni mwa wapinzani watatu waliyobaki kwa sasa kumpa changamoto Sepp Blatter kabla ya uchaguzi mwezi Mei.
Na wakati wa uzinduzi wa kampeni yake Prince Ali, ambaye ni mgombea anayesaidia mara kwa mara vyama vya soka, alidai atapambana haki.
"Kumekuwa na utamaduni wa vitisho ndani FIFA," alisema Bosi huyo mwenye umri wa miaka 39.
"Ni wazi madarakani yana faida ki asili lakini nataka kuwahakikishia vyama vya kitaifa kuwa tutasonga mbele katika mwelekeo sahihi." alifafanua Prince Ali Bin Al Hussein
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments