Ticker

6/recent/ticker-posts

Soma alichokisema kocha wa Southampton Ronald Koeman kuhusu Champions League baada ya timu yake kutoka sare na Aston Villa usiku wa kuamkia leo

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.NOV.25,2014 SAA 10:31 USIKU
Nathaniel Clyne scored a late equaliser for Southampton as they drew 1-1 away at Aston Villa on Monday night
Ligi kuu nchi England imeendelea Usiku wa kuamkia hii leo kwa mchezo mmoja kati ya Aston Villa
na Southampton,mchezo uliopigwa katika dimba Aston Villa  maalufu kama Villa Park,mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Katika mchezo huo Aston Villa ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mchezaji wake ambaye ni raia wa nchini huo ,Gabriel Agbonlahor mnamo katika dakika ya 29 ya mchezo huo,baada ya walinzi wa klabu ya Southampton kufanya makosa.

Southampton walizinduka katika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata bao la kusawaisha kupitia kwa Nathaniel Clyne,kunako katika dakika ya 81 ya mchezo huo.
Clyne (second left) equalised for the visitors in the final few minutes of the match with a sweetly-struck side-footed shot
Mara baada ya mchezo huo kumalizika,Meneja  wa Southampton, Ronald Koeman amesisitiza kuwa timu yake inaweza kumaliza katika nafasi nne za juu kwa msimu huu licha ya kutoka kwa sare ya 1-1 na Aston Villa siku ya jana,katika Monday Night Football.

Ingawa sare hiyo imewafanya washindwe kusogea,bado Southampton wako katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi,na alama saba- juu kwa Newcastle United ambao wapo katika nafasi ya tano .

Alipoulizwa kama anadhani timu yake inaweza kufuzu na kucheza Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza msimu huu,Meneja  wa Southampton, Ronald Koeman,alikuwa na haya ya kusema.

 "Ndiyo Nadhani inawezekana,kwa sababu Sioni timu nyingi nyingine zenye ubora kuliko Southampton.

"Tutacheza vizuri kuliko usiku wa leo lakini kila mtu anajua Premier League ni vita kila mchezo, na kuna timu kubwa ambazo zinapambana,Kama sisi tutaendelea kwenda hivi, kuwa na nguvu na tabia nzuri  katika timu iliyoonekana leo, nafikiri inawezekana. " alisema Meneja  wa Southampton, Ronald Koeman.

MARA BAADA YA MCHEZO HUO, SASA MSIMAMO WA LIGI KUU ENGLAND UKO KAMA IFUATAVYO.

England - Premier League - Table
#
Team NamePWDLFAGDPts
1
Chelsea12102030111932
2
Southampton128222461826
3
Manchester City1273224131124
4
Manchester United125431915419
5
Newcastle United125431415-119
6
West Ham United125342016418
7
Swansea City125341613318
8
Arsenal124532015517
9
Everton124532219317
10
Tottenham Hotspur125251617-117
11
Stoke City124351315-215
12
Liverpool124261518-314
13
West Bromwich Albion123451317-413
14
Sunderland122731219-713
15
Crystal Palace123361721-412
16
Aston Villa12336617-1112
17
Hull City122551417-311
18
Leicester City122461118-710
19
Burnley12246820-1210
20
Queens Park Rangers122281123-128

KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments