Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.OCT.12,2014 SAA 04:52 USIKU
Timu ya taifa ya Uganda Uganda The Cranes imepokea kipigo cha 1-0 kutoka kwa Timu ya Togo katika mchezo uliopigwa katika
uwanja wa Mandera mjini Kampara Uganda.
Bao la Togo liliwekwa kimyani katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wao Donou Kokou baada ya kupokea pasi kutoka kwa Emmanuel Adebayor.
Kipindi cha pili kocha wa Uganda Cranes Milutin Sredojevic "Micho" alifanya mageuzi kwa nia ya kutaka kupata goli la kusawazisha,kwa kumuondoa Moses Oloya,Luwaga William Kizito na Khalid Aucho na kumuingiza Emmanuel Okwi,Brian Umony na Brian Majwega hata hivyo mabadiliko hayo hayakuzaa matunda mema kwa Uganda Cranes.
Ushindi wa Togo unawarudisha kwenye jedwali la kufuzu kucheza fainali kama watapata ushindi katika mechi ya Jumatano dhidi ya Uganda katika mchezo wa marudiano utakaopigwa nchini Togo.
Emmanuel Adebayor akijifua kabla ya mechi |
Kikosi cha Uganda Cranes kikiwa katika mazoezi |
Uganda Cranes haijawai kufungwa katika uwanja wao wa Nyumbani kwa kipindi cha miaka 10 baada ya kufungwa na Afrika kusini mwaka 2005,na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Poul sali anaaminika katika mchezo huo wachezaji wa Uganda waliamini Historia hiyo na kujisahau.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments