Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.OCT.12,2014 SAA 04:52 USIKU
Timu ya soka ya Tanzania imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4 - 1 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa
katika dimba la taifa jijini Dar es salaam.
katika dimba la taifa jijini Dar es salaam.
Mpaka mchezo unamaliza kipindi cha kwanza Tanzania ilikuwa inaongoza kwa mabao mawili kwa sifuri katika mchezo huo ilochezeshwa na refa Hakizimana Loius.
Bao la kwanza la Tanzania lilifungwa kwa kichwa na Nadir Haroub "Cannavaro" katika dakika ya 17 ya mchezo huo, kwa kuunganisha kona iliyochongwa na Erasto Edward.
Bao la pili la Stars lilikwamishwa nyavuni na Kiungo Amri Kiemba dakika ya 40 ya mtanange huo,ambapo baadaye mchezeaji huyo alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Abubakar.
Kipindi cha pili Benin walifanya mabadiliko ya kipa kwa kumtoa Farnoue Fabien na kumuingiza Allagbe Saturnin lakini Taifa stars bado ikafanikiwa kudumbukiza mabao mengine mawili.
Na mabao hayo yalifungwa na Mshambuliaji wa Tanzania anayechezea TP mazembe ya Jamuhuli ya kidemokrasia ya Kongo Thomas Ulimwengu katika dakika ya 48 baada ya kuunganisha Krosi kutoka kwa Mrisho Ngassa,na msumali wa mwisho wa Stars ulishindiliwa na mshambuliaji wake anayechezea timu ya ZESCO United ya Zambia Juma Luis ambaye ndiye aliyechukuwa nafasi ya Ngassa aliyetolewa katika dakika ya 14 ya kipindi cha pili.
KIKOSI TAIFA STARS
KIKOSI BENIN
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
Amri Kiemba akisangilia bao la pili |
KIKOSI BENIN
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments