NA MWANDISHI WETU,TANGA. IMEWEKWA.OCT.08,2014 SAA 01:30 USIKU
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema utakwenda mahakamani
kuishtaki Kampuni ya Binslum Tyre
kutokana na kitendo cha kutengeneza tisheti za Coastal Union zenye nembo ya kampuni Sound na kuwapa bure mashabiki kuingiza nazo kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara wakiwa wamelipiwa na viingilo vya mchezo husika.
kutokana na kitendo cha kutengeneza tisheti za Coastal Union zenye nembo ya kampuni Sound na kuwapa bure mashabiki kuingiza nazo kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara wakiwa wamelipiwa na viingilo vya mchezo husika.
Hali hiyo
ni kinyume na utaratibu kutokana na kuwa tayari kampuni hiyo
ilishajitoka kufadhili timu hiyo na tayari klabu ya Coastal Union
ilikwishapata mfadhili mwengine ambayo ni kiwanda cha Kutengeneza Unga
Ngano mkoani Tanga cha Pembe Flours Mills.
Kauli hiyo imetolewa
kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji Kilichoketi mwishoni mwa wiki ambapo
kilikuwa na agenda nne za msingi ambazo ni Suala la mshambuliaji wa
Coastal Union Danny Lyanga,Utoaji slipi benki,Jezi za Sound,Tarehe ya
Uchaguzi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal
Union,Steven
Mguto,Katibu Mkuu Kassim El Siagi,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji,Albert
Peter Saimu Amiri na Meneja wa Coastal Union Akida Machai.
Kimsingi
suala ambalo lilikuwa gumzo ni suala la kampuni hiyo kuchukua hatua ya
kuwavalisha mahsbiki wa Coastal Union jezi pamoja na kuwalipia viingilio
vya mechi kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu.
Kama unavyojua
kuwa Kampuni ya Binslum Tyres ilikuwa mhisani wetu na sasa hatuko naye
na tayari alishapeleka fedha zake kwenye vilabu vingine ikiwemo Mbeya
City sasa tunamshangaa kuendelea kufanya biashara ya matangazo kupitia
mashabiki wetu kwa kuwapa tisheti za kuvaa bure ikiwemo kuwalipia
viingilio kwenye mechi za ligi kuu zinazochezwa Mkwakwani.
Hivyo
kutokana na suala hilo tayari uongozi wa Coastal Union umeshamkamata
mshabiki mmoja ambaye ni wakala wa kusambaza tisheti hizo kwa mashabiki
na kumpeleka polisi na taratibu za kisheria zinaendelea ili kuweza
kukomesha vitendo hivyo ambavyo sio vya kiungwana.
Tayari Kampuni
ya Pembe Flours Mills ilishasaini mkataba na Klabu ya Coastal Union wa
kufadhili kwa kipindi cha mwaka mmoja hivyo Kampuni hiyo kuendelea
kufanya matangazo yake kupitia mashabiki hao ni kuvunja utaratibu
uliokuwepo.
Hata hivyo tayari Pembe walishatoa jezi 2000 kwa
ajili ya kuziuza kwa masabiki mbalimbali wa soka jijini Tanga zilizokuwa
na nembo ya pembe na TSN.
Kuhusu suala la Uchaguzi wajumbe wa Kamati
hiyo walikubaliana uchaguzi huo ufanyika Novemba 23 mwaka huu ambapo
nafasi zitakazojazwa ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo na wajumbe wawili wa
kamati ya utendaji
Suala la Utiliaji Sahihi wajumbe
walilipendekeza fedha zitumike kwenye matumizi yanayofahamika ikiwemo
kuwekwa utaratibu wa wazi kwenye matumizi husika.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments