Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.OCT.08,2014 SAA 03:04 USIKU
Add caption |
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema Shinji Kagawa "alionyesha matumaini
madogo" baada ya Juan Mata kuwasili kaika klabu hiyo mwezi January.
Ferguson alimleta Kagawa Old Trafford kutoka Borussia Dortmund mwaka 2012, lakini mchezaji huyo amerejea tena Ujerumani mwezi Agosti baada ya misimu miwili migumu nchini England.
David Moyes aliyewasili baada ya kustaafu kwa Ferguson, mara nyingi alimtumia Kagawa upande wa kushoto wa kiungo kuliko katika jukumu lake kuu, na alifanya usajili wa Mata, pia No.10, kwa rekodi ya klabu £37 million.
Louis van Gaal, ambaye alibadilishwa baada ya Moyes kutimuliwa kama meneja, alifanya uamuzi wa kumuacha Kagawa baada ya kuchukua utawala katika klabu ya Manchester, lakini Ferguson anaamini maamuzi hayo yalifanyika mara baada ya kusajiliwa kwa Mata.
"Kila meneja wa ana falsafa yake mwenyewe. Wakati Moyes anamsaini Nyota wa Hispania Mata, Kagawa aliona kwamba hatakuwa tena chaguo la kwanza, na akaonesha matumaini madogo," aliiambia Bild.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments