Ticker

6/recent/ticker-posts

WATU 70 WA KWANZA MECHI YA AZAM NA YANGA KUINGIA BURE

Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Sept.10,2014 SAA 02:05 USIKU
Shorikisho la soka nchini Tanzania limetangaza viingilio vya mechi ya Ngao ya Jamii,mchezo ambao inaashiria uzinduzi
wa msimu mpya wa Ligi kati ya Azam na Yanga itakayochezwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kiingilio cha chini kabisa katika mchezo huo ni sh. 5,000.

Viingilio vingine katika mechi hiyo ambayo itatumia tiketi za elektroniki ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa viti vya VIP C na B wakati viti vya VIP A kiingilio ni sh. 30,000.

Kaimu katibu mkuu wa Tff,Boniface Wambura ameiambia Duru za Michezo kuwa lengo la mchezo huo ni kusaidia Jamii,na safari hii itakuwa ni kusaidia mfuko wa damu salama,na watu 70 wa kwanza watakaoweza kuchangia damu wataweza kuingia Bure katika mchezo huo na kukaa katika viti maalum (VIP).

Wachezaji wa Azam Fc wakijifua
"tutakuwa na watu wa Damu salama ambao ni moja ya watu tutakaowasaidia katika hii mechi,siku ya mechi kutakuwa na fursa ya watu kuchangia damu,na sisi kama Tff tumesema watu 70 wa kwanza kuchangia damu watapata tiketi ya bure ya moja kwa moja kuingia uwanjani,utararibu utakuwa ni ule ule kama uliozoeleka,kama ukishachangia damu ukitaka kuongeza damu kwa maji,soda au maziwa utapatiwa"

"kwa hiyo tunasisitiza watu kujitokeza kwani  Tanzania kunaupungufu wa damu salama,na watu wa damu salama,wanalengo la kusaidia watu,kwani sio kila mtu anayepata ajali na kupoteza damu anauwezo wa kupata damu moja kwa moja"alisema Boniface Wambura

Mwaka jana kupitia Mechi ya Ngao ya jamii Tff ilinunu kitanda cha kufanyia upasuaji katika hospitali ya Temeke,kwa sababu ipo karibu na uwanja wa taifa ambapo kama ikitokea mtu ameumia basi anapelekwa katika hospitali hiyo.

KWA TAARIFA,MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,BREAKING NEWS,LIKE PAGE YA FACEBOOK  BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .

Post a Comment

0 Comments