Timu
ya soka ya Mbeya city jumamosi hii inataraji kucheza mchezo wa kimataifa wa
kujipima nguvu dhidi ya timu ya
Vipers Fc zamani bunamwanya inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uganda mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya.
Vipers Fc zamani bunamwanya inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uganda mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya.
Akiongea
na Jamii na Michezo afisa habari wa Mbeya City Dismas Ten amesema kuwa kikosi hicho
kinataraji kutua jijini Mbeya ijumaa ya kesho kikiwa na msafara wa watu 25
viongozi 5 na wachezaji 20.
Ten
ameongeza kuwa timu hiyo iana taraji kwa kipimo kizuri kwa timu ya Mbeya City
kwani mmoja ya timu ambazo zimeonyesha uwezo mkubwa katika ligi ya Uganda na
kufanikiwa kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya nchi hiyo.
Huu
utakuwa mchezo wa mwisho wa kujipama nguvu kwa Mbeya City kabla kuanza mbilinge
la ligi kuu ya soka Tanzania bara inayotaraji kuanza kutimua vumbi September 20
kwenye viwanja mbalimbali.
Mbeya
city ambayo ilikamata nafasi ya tatu msimu uliopita kwenye ligi kuu ya soka
Tanzania bara inaendelea na mawindo yake chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi na
msaidizi wake Suleiman Jabir
Afisa
habari wa Mbeya City Dismas Ten amewaomba wakazi wa Mbeya kujitokeza kwa wingi
katika mchezo huo jumapili kuishuhudia timu yao pendwa ikionyesha kile ambacho
imejipanga nacho kwa ajili ya ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka
2014/2015.
KWA TAARIFA,MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,BREAKING NEWS,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
KWA TAARIFA,MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,BREAKING NEWS,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments