Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Sept.15,2014 SAA 02:15 USIKU
Mshambuliaji wa Zamani wa Real Madrid na Chelsea Nicolas Anelka ametangaza kuwa amejiunga na klabu ya Mumbai
City inayoshiriki ligi ya India inayojulikana kama Indian Super League.
Kulikuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 , alikuwa hana klabu tangu aondoka West Brom kufuatia kupigwa marufuku kwa kuonesha ishara ya kibaguzi.
Lakini Anelka anaweza kuchelewa kuichezea timu hiyo ya india maada ya FA kusema kuwa mchezaji huyo hataweza kuitumikia klabu hiyo mpaka adhabu yake ya kufungiwa mechi tano itakapo kamilika.
Lakini Anelka anaweza kuchelewa kuichezea timu hiyo ya india maada ya FA kusema kuwa mchezaji huyo hataweza kuitumikia klabu hiyo mpaka adhabu yake ya kufungiwa mechi tano itakapo kamilika.
"Nimefurahi kujiunga na Mumbai City FC & nimepata hamasa sana kujiunga na Indian Super League" Anelka aliandika katika Twitter.
"Ina wachezaji wenye vipaji vya kimataifa & vipaji vya hali ya juu vya India itanifanya kucheza mechi kwa furaha kubwa".
"Mimi naangalia mbele kwa kutumia uwezo wangu wa kufanya vizuri kwa timu yangu katika mechi tutakazocheza."
Anelka, amejitokeza mara 69 katika mechi za Ufaransa, alianza kazi yake na Paris St Germain kabla ya kujiunga na Arsenal , akaenda kucheza katika klabu ya Real Madrid, Manchester City, Fenerbahce, Liverpool, Bolton, Chelsea, Shanghai Shenhua, Juventus na West Brom na mara nyingi kuamekuwa akihamahama na kufanya kazi yake ipande na kushuka.
KWA TAARIFA,BREAKING NEWS,RATIBA PAMOJA NA MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments