Mhariri:Herman Kihwili IMEWEKWA.Aug.10,2014 SAA 03:57 USIKU
WANACHAMA wa Klabu ya Coastal
Union ya Tanga wamemdumaza kiutendaji (Dormant Leader) kwenye shughuli za
kila
siku kwenye klabu hiyo Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Steven Mguto kutokana
na uvunjaji wake wa katiba ya klabu hiyo kitendo ambacho kimewafanya wanachama
hao kukosa imani naye.
Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya
wanachama hao,Zuberi Unenge alisema kuwa wao hawamfukuzi makamu mwenyekiti wa
Coastal Union Steven Mguto kwa kufanya hivyo itakuwa wamekiuka taratibu za
viongozi waliochaguliwa kwa kura na wanachama ambao hawapaswi kuondolewa madarakani
kwa mujibu wa katiba.
Alisema kuwa kwa kuwa kiongozi
huyo hafuati katiba ya Coastal Union na huwa anaivunja Katiba hiyo kila mara
wameonyesha kuwa na wasiwasi naye katika utendaji wake kwa ajili ya maendeleo
klabu hiyo.
Katika baadhi ya sababu
walizomshutumu nazo ni suala la uhamisho wa mchezaji Ibrahimu Twaha “Mesi” na
Abdi Banda kwa kauli alizotoa kwenye vyombo vya habari akithibitisha kuwa
habari hizo zinaukweli wakati ni yeye aliyeidhinisha wachezaji hao kupewa
mishahara mwezi mei na juni akiwa kama makamu mwenyekiti wa Coastal Union na
wachezaji wakapewa.
Aidha pia walimshutumu kwa kauli
aliyeitoa kwenye mitaa ya kijamii ya kuwa yeye hajisikii kuwa kiongozi ndani ya
klabu ya Coastal Union akiwa anaungana mkono na wapinzani wasioitakia mema
klabu hii.
“Sisi kama wanachama tunashangazwa sana na kiongozi wa aina hii ambaye
yeye anaangalia maslahi yake binafsi na sio timu hiyo nadhani tukiendelea kuwa
naye anaweza kutufikisha mahali pabaya hasa kwa sababu timu ipo Tanga nay eye anaishi
Dare s Salaam “Alisema Unenge.
Kwa kuwa suala hilo la kumdumaza kiongozi
ni jipya kwa hiyo wanachama hao walitumia kifungu cha sita masharti ya muda na
ya mwisho ibara ya 57 kinachoelezea masuala ambayo hayamo kwenye katiba
kisheria kuiamuru kamati ya utendaji kuwasiana na TFF kupata ufafanuzi wa
kisheria kuhusu jambo hilo wakati utekelezaji wa kumdumaza kiongozi hiyo ukiwa
unaendelea.
0 Comments