Manchester City wamethibitisha kwamba mshambuliaji Sergio Aguero amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na
klabu hiyo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amejifunga kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu hadi mwishoni wa msimu 2018/19 na amesaini mkata mpya siku moja tu baada nahodha wa City Vincent Kompany pia kuongeza mkataba mpya wa miaka mitano .
Aguero alifurahishwa mno kwa kujua mustakabali wake huo kabla ya kuanza kwa msimu mpya, na ana furaha kwa kumaliza uvumi ulioenea juu yake kuwa atarudi La Liga.
Aguero aliiambia tovuti rasmi ya klabu hiyo: "Ukweli unaonekana kuwa tangu nimekuja hapa, kila wakati wa kumaliza msimu, kumekuwa kuna uvumi na unapendekeza kuwa nirudi Hispania"
" daima kumekuwa na uvumi huu,lakini mimi niko makini sana na hilo".
"Watu husikia mambo haya na wao wanachukulia kwa umakini lakini nawaambia mashabiki na kila mtu wa Man City wasiwe na hofu, nitakuwa hapa mpaka mkataba wangu umalizike".
0 Comments