Meneja wa Crystal Palace Tony Pulis amesitisha jukumu lake la ukocha na klabu hiyo baada ya mazungumzo na
mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Parish jijini London siku ya Alhamisi jioni.
Pulis alisimamia mafunzo, kama vile kumsajili beki wa Liverpool Martin Kelly, mapema katika siku za hivi karibuni kisha inaaminika kuwa alisafiri kwenda hoteli iliyopo katikati ya jiji la London kwa ajili ya mkutano na Steve Parish.
Bosi huyo wa zamani wa Stoke iliripotiwa kuwa na msuguano na bodi kuu ya klabu juu ya shughuli zao katika soko uhamisho msimu huu, baada ya kuwakosa wachezaji kadhaa walio katika malengo yake .
Tony Pulis ameweza kukamilisha usajili wa Kelly, Brede Hangeland na Frazier Campbell, lakini inaonekana kuwa Pulis hakuwa na furaha na kikosi chake siku mbili tu kabla ya wao kuanza msimu mpya dhidi ya Arsenal - Keith Millen unatarajiwa kuwa meneja wa muda na kuongoza kikosi cha Crystal Palace katika uwanja wa Emirates.
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments