TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga kesho inatarajiwa
kucheza mechi ya kirafiki na Handeni City mchezo unaotazamiwa kuchezwa
kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea
msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara.
Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani hapa,Ofisa habari wa
Coastal Union Oscar Assenga amesema mchezo huo utaanza kesho saa kumi
jioni lengo likiwa ni kujenga undugu baiina ya timu zote mbili.
Assenga
amesema katika mchezo huo kikosi kinachotazamiwa kushiriki ligi kuu
msimu ujao kinaonyesha makali yake kwenye mchezo huo.
Aidha mashabikki wa soka mkoani hapa wametakiwa kujitokeza kwa
wingi ili kuweza kushuhudia mchezo huo ambao utakuwa mkali na wa
kusisimua.
0 Comments