Winga wa Bayern Munich Franck Ribery ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa na timu yake ya taifa ya
Ufaransa.
Ribery ameshinda 82 vikombe akiwa mwandamizi wa Ufaransa tangu mwaka 2006 lakini amekosa msimu huu wa Kombe la Dunia baada ya kushindwa kupata nafuu kutokana na tatizo sugu la mgongo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 sasa amesema anahisi ni wakati muafaka wa kuwaruhusu wachezaji vijana kuchukuwa nafasi hiyo na yeye anataka kutumia muda zaidi akiwa na Bayern Munich pamoja na familia yake.
"Niliutafuta huu wakati," aliiambia kicker. "Nataka kujitolea zaidi kwa familia yangu na kuwa makini na kazi katika klabu ya Bayern, na pia naondoka katika sehemu ya timu ya taifa kwa sababu ya wachezaji wengi vijana wazuri".
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
ILI KUWEZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI,LIKE PAGE YA FACEBOOK BONYEZA HAPA (Jamii na Michezo) .
0 Comments